Viongo vya kutumia
- Nyama 1kg
- Nyanya 2kubwa
- Pilipili hoho 1kubwa
- karoti 1kubwa
- Thomu iliyo sagwa 1 kijiko cha chai
- Tangawizi iliyo sagwa 1kijiko cha chai
- Chumvi kiasi
- Kitunguu maji 1kikubwa
- Royco packiti moja
- chukua nyama yako ikatekate vipande unavyo itaji,na uioshe iwe safi.
- kisha iweke tangawizi ambayo umesha isaga changanya na iweke chumvi kiasi na uibandike jikoni ,usubili mpaka iive vizuri ,na uiipue ikiwa imeiva.
- Bandika sufuria na uweke mafuta kiasi,na yakipata moto weka vitunguu vyako vikaange mpaka vibadilike rangi na uweke hoho na karoti navyo vichanganye
- kisha chukua nyanya nazo zitie kwenye ule mchanganyiko woko, koroga nyanya baada ya muda kidogo weka thomu zako nazo zichanganye na ile rost yako ya nyanya
- baada ya muda kidogo weka nyama yako na uikaange na ile lost ya nyanya, subili kwa muda kidogo kisha weka ile supu ambayo ulichemshia nyama ichanganye na isubili hadi maji yakauke kidogo kisha weka royco nayo ichanganye kisha isubili na ukionja chumvi kama imekolea ,na hapo lost lako litakuwa tayali kwakuliwa na chakula chochote.