Wednesday, October 2, 2013

MCHUZI WA SAMAKI WA NAZI.

Leo tutajifunza jinsi ya kupika mchuzi wa samaki wa Nazi,

VIPIMO
  • Samaki wa vipande   3-4 vikubwa
  • kitunguu maji kikubwa    1
  • Nyanya                             2
  • Tui zito la Nazi                 2 vikombe
  • Binzali ya  manjano           1/4 kijiko cha  chai
  • Thomu                                 kiasi
  • Hoho                                   1
  • karoti                                   1
  • chumvi                                 kiasi
  • Pili pili                                 2
VIPIMO VYA SAMAKI NA NAMNA YA KUWATAYA
RISHA
  • Thomu iliyosagwa              1 kijiko
  • Abdalasini ya unga             1/2 kijiko
  • Ndimu za maji                     2
  • Chumvi                                kiasi
  • Tangawizi iliyosagwa          1 kijiko
  • Mafuta ya kukaangia samaki  1 chupa 
  JINSI YA KUPIKA
1.Andaa moto wako uwe wa jiko la mkaa,mchina au la umeme

2.Tayarisha frampeni kwa ajili ya kukaangia samaki,weka mafuta jikoni yakisha pata moto weka samaki na wakaange wakauke vizuri.

3.Tayarisha viungo vyako kuna Nazi,menya nyanya,hoho na karoti.

4.Weka sufuria yako jikoni

5.Ikipata moto weka mafuta kiasi ili kukaangia viungo vyako

6.Mafuta yakiwa tayari anza kukaanga vitunguu

7.Hakikiasha vimebadilika rangi kuwa brauni weka karoti

8.Vikiwa tayari weka hoho

9.Vikisha kaangika vizuri weka kitunguu thomu  

10.Baada ya hapo weka nyanya zikaangike vizuri halafu weka na chumvi kiasi

11.Zikisha kaangika weka binzari ya njano kasha koroga vizuri ichanganyike weka na pili pili kwa ajili ya kupa test ya kula.

12Baada ya hapo weka tui zito na ukoroge hadi lichemke

13. Likisha chemka vizuri weka vipande vya samaki kisha wakoroge vizuri onja na chumvi kama iko sawa subiri baada ya dakika mbili mchuzi wako utakuwa taayar kuliwa na chochote uwe wali,ugali ,mkate na chapatti.

No comments:

Post a Comment