Sunday, September 29, 2013

JINSI YA KUPIKA PILAU LA NYAMA YA NG`OMBE

                                                                                                                                                                                                          
 Karibu katika jiko na mapishi, na leo tutajifunza kupika pilau la nyama ya ng`ombe.
  VIPIMO,
  • Mchele 2kg
  • Nyama ya ng`ombe 1k
  • Pilpilihoho 1kubwa
  • Nyanya  3kubwa
  • Vitungu maji 2vikubwa
  • Thomu iliyosagwa 1kimoja cha supu
  • Tangawizi 1kijiko kimoji cha chai
  • Mafuta ya kupikia 1/2 kikombe
  • Binzari nyembamba 1kijiko kimoja cha chai
  • Pilpili manga1/2 kijiko cha chai
  • Hiliki 1/2 kijiko cha chai           
JINSI YA KUPIKA PILAU LA NYAMA YA NG`OMBE
  1. Loweka mchele wako katika chombo,
  2. Chukua nyama na uioshe na itie thomu,tangawizi,ndimu,pilipili manga, na chumvi kiasi
  3. Iweke jikoni hadi ikauke maji,na maji yakikauka  ikaangekaange ka hayo hayo mafuta ambayo uliyaweka mwanzo hadi kuwa rangi ya hudhurungi(broun)
  4. Katakata vitunguu na nyanya pembeni
  5. Chukua pilpil manga,thomu,tangawizi na uvisage katika mashine ya kusagia au kinu,
  6. Weka sufuria jikoni  na utie mafuta,subili yapate moto,
  7. Kisha tia vitungu na vikaange hadi kuwa hudhurungi  na tia nyanya
  8. Kisha mimina mchanganyaiko wako ulio usaga na pilpil mang  thomu na tangawizi, 
  9. Koroga kwa dakika kathaa kisha mimina nyama iliyokuwa tayali maji kisha na chumvi kidogo  nasubili maji yachemke na weka mchele wako uchanganye vizuri ili uchanganyike na viungo vyako pamoja na nyama isikae sehemu moja 
  10. Funika hadi maji yakauke,na ugeuze kama umeiva kama bado ufunike tena,subili kw dakika chake, na hapo chakula chako kitakuwa tayali kwa kuliwa 
    Ili ndilo pilau la nyama ya ng`ombe,liko teyali kwa kuliwa na kachumbali au na chochote kile.