Wednesday, October 2, 2013

ROST YA NYAMA

karibu tena kwenye jiko na mapishi na tunajifunza kupiki lost ya nyama.
Viongo  vya kutumia
  • Nyama   1kg
  • Nyanya   2kubwa
  • Pilipili hoho  1kubwa
  • karoti    1kubwa
  • Thomu iliyo sagwa    1 kijiko cha chai
  • Tangawizi iliyo sagwa  1kijiko cha chai
  • Chumvi     kiasi
  • Kitunguu maji  1kikubwa
  • Royco    packiti moja
JINSI YA KUPIKA ROST YA NYAMA
  1. chukua nyama yako ikatekate vipande unavyo itaji,na uioshe iwe safi.
  2. kisha iweke tangawizi ambayo umesha isaga  changanya na iweke chumvi kiasi na uibandike jikoni ,usubili mpaka iive vizuri ,na uiipue ikiwa imeiva.
  3. Bandika sufuria  na uweke mafuta kiasi,na yakipata moto weka vitunguu vyako vikaange mpaka vibadilike  rangi na uweke hoho na karoti  navyo vichanganye
  4. kisha chukua nyanya  nazo zitie kwenye ule mchanganyiko woko, koroga nyanya  baada ya muda kidogo weka thomu zako nazo zichanganye  na ile rost yako ya nyanya
  5. baada ya muda kidogo weka nyama yako na uikaange na ile lost  ya nyanya, subili kwa muda kidogo  kisha weka ile supu ambayo ulichemshia nyama  ichanganye  na isubili hadi maji yakauke kidogo kisha weka royco nayo ichanganye  kisha isubili na ukionja chumvi kama imekolea ,na hapo lost lako litakuwa tayali kwakuliwa  na chakula chochote.

MCHUZI WA SAMAKI WA NAZI.

Leo tutajifunza jinsi ya kupika mchuzi wa samaki wa Nazi,

VIPIMO
  • Samaki wa vipande   3-4 vikubwa
  • kitunguu maji kikubwa    1
  • Nyanya                             2
  • Tui zito la Nazi                 2 vikombe
  • Binzali ya  manjano           1/4 kijiko cha  chai
  • Thomu                                 kiasi
  • Hoho                                   1
  • karoti                                   1
  • chumvi                                 kiasi
  • Pili pili                                 2
VIPIMO VYA SAMAKI NA NAMNA YA KUWATAYA
RISHA
  • Thomu iliyosagwa              1 kijiko
  • Abdalasini ya unga             1/2 kijiko
  • Ndimu za maji                     2
  • Chumvi                                kiasi
  • Tangawizi iliyosagwa          1 kijiko
  • Mafuta ya kukaangia samaki  1 chupa 
  JINSI YA KUPIKA
1.Andaa moto wako uwe wa jiko la mkaa,mchina au la umeme

2.Tayarisha frampeni kwa ajili ya kukaangia samaki,weka mafuta jikoni yakisha pata moto weka samaki na wakaange wakauke vizuri.

3.Tayarisha viungo vyako kuna Nazi,menya nyanya,hoho na karoti.

4.Weka sufuria yako jikoni

5.Ikipata moto weka mafuta kiasi ili kukaangia viungo vyako

6.Mafuta yakiwa tayari anza kukaanga vitunguu

7.Hakikiasha vimebadilika rangi kuwa brauni weka karoti

8.Vikiwa tayari weka hoho

9.Vikisha kaangika vizuri weka kitunguu thomu  

10.Baada ya hapo weka nyanya zikaangike vizuri halafu weka na chumvi kiasi

11.Zikisha kaangika weka binzari ya njano kasha koroga vizuri ichanganyike weka na pili pili kwa ajili ya kupa test ya kula.

12Baada ya hapo weka tui zito na ukoroge hadi lichemke

13. Likisha chemka vizuri weka vipande vya samaki kisha wakoroge vizuri onja na chumvi kama iko sawa subiri baada ya dakika mbili mchuzi wako utakuwa taayar kuliwa na chochote uwe wali,ugali ,mkate na chapatti.

Sunday, September 29, 2013

JINSI YA KUPIKA PILAU LA NYAMA YA NG`OMBE

                                                                                                                                                                                                          
 Karibu katika jiko na mapishi, na leo tutajifunza kupika pilau la nyama ya ng`ombe.
  VIPIMO,
  • Mchele 2kg
  • Nyama ya ng`ombe 1k
  • Pilpilihoho 1kubwa
  • Nyanya  3kubwa
  • Vitungu maji 2vikubwa
  • Thomu iliyosagwa 1kimoja cha supu
  • Tangawizi 1kijiko kimoji cha chai
  • Mafuta ya kupikia 1/2 kikombe
  • Binzari nyembamba 1kijiko kimoja cha chai
  • Pilpili manga1/2 kijiko cha chai
  • Hiliki 1/2 kijiko cha chai           
JINSI YA KUPIKA PILAU LA NYAMA YA NG`OMBE
  1. Loweka mchele wako katika chombo,
  2. Chukua nyama na uioshe na itie thomu,tangawizi,ndimu,pilipili manga, na chumvi kiasi
  3. Iweke jikoni hadi ikauke maji,na maji yakikauka  ikaangekaange ka hayo hayo mafuta ambayo uliyaweka mwanzo hadi kuwa rangi ya hudhurungi(broun)
  4. Katakata vitunguu na nyanya pembeni
  5. Chukua pilpil manga,thomu,tangawizi na uvisage katika mashine ya kusagia au kinu,
  6. Weka sufuria jikoni  na utie mafuta,subili yapate moto,
  7. Kisha tia vitungu na vikaange hadi kuwa hudhurungi  na tia nyanya
  8. Kisha mimina mchanganyaiko wako ulio usaga na pilpil mang  thomu na tangawizi, 
  9. Koroga kwa dakika kathaa kisha mimina nyama iliyokuwa tayali maji kisha na chumvi kidogo  nasubili maji yachemke na weka mchele wako uchanganye vizuri ili uchanganyike na viungo vyako pamoja na nyama isikae sehemu moja 
  10. Funika hadi maji yakauke,na ugeuze kama umeiva kama bado ufunike tena,subili kw dakika chake, na hapo chakula chako kitakuwa tayali kwa kuliwa 
    Ili ndilo pilau la nyama ya ng`ombe,liko teyali kwa kuliwa na kachumbali au na chochote kile.

Friday, August 30, 2013

LEO TUTAJIFUNZA JINSI YA KUPIKA WALI WA ILIKI PAMOJA NA MAALAGE NA SOSEJI

VIFAA VYA KUTUMIA
  1. mchele 1kg
  2. maharage nusu
  3. mafuta ya kupikia nusu
  4. iliki pakiti moja
  5. nazi moja
  6. soseji pakiti moja
  7. chuvi
  8. kitungu maji kimoja
HATUA YA KUPIKA MBOGA
  • Unachukua sufuria yako unaiweka jikoni kisha unaweka mafuta kwenye sufuria,mafuta yakipata moto utaweka vitungu maji na kuvikaanga mpaka viwe vya broun, kisha utaweka maharage yako ulio yachemsha kabisa,na kuchanganya na vile vitungu kisha vikisha changanyika unaweka tuila la nazi lile la pili,lile tui likichemka unaweka la pili pamoja na zaizi utakayo itaka ya chumvi,utasubili baada ya dakika tono utaonja chumvi kama,kisha utatoa mboga yako jikoni ikiwa imeiva na yakupendeza. 

    hipicha inaonyesha  mboga ikiwa tayali kwa kuriwa na chochote ugali,wali

    

    hiki ndicho chakula chetu tulicho pika

    

    

     

HATUA YAKUPIKA WALI WA ILIKI
  • Kwanza kabisa unatakiwa kuanda mchele wako, upepete ili kutoa uchafu kisha utautia kwenye maji ili kuosha  kisha utainjika sufuria ya wali  kwenye moto kisha utaweka maji ambayo yatatosha mchele wako,nakuweka chumvi na iliki iliyo sagwa, nakufunika haya maji,badaaa ya maji kuchemka utaweka mchele ulio uosha tayali n kuchanganya maji na ulimchele uku ukionja chumvi kama imekolea kisha utafunika ukisubilia maji yakauke,baada ya dakika kama moja unaangalia kama maji yamekauaka, kama yamekauka  utaugeuza ili pande zote ziive,utafunika kw maro  ya pili ,baada ya muda kidogo chakula kitakuw kimeiva,na kiko tayali kwakula,huku ukizisubili soseji zako zikiwa kwenye maji ya moto au mafuta.Hadi hapo chakula kitakuwa kimeiva na kipo tayali  kwa kuliwa

Chakula kiko tayari kwa kuliwa

   

.

KARIBU KWENYE JIKO NA MAPISHI

Huhu ni muonekano wa jiko la kisasa ambalo unaweza kupikia ukiwa na amani

Hiki ni chakula ambacho kila mtu anaweza kukila,kwa muda wa mchana hata usiku.